1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mawaziri wa EU kukutana na kuijadili Ukraine na Gaza

22 Julai 2024

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanakutana leo Jumatatu kujadili migogoro inayoendelea nchini Ukraine na Mashariki ya Kati.

https://p.dw.com/p/4iaDX
Brussel, Ubelgiji |  Josep Borrell
Katibu Mkuu wa Sera za Kigeni Umoja wa Ulaya Josep Borrell Picha: Lenoir/EUC/Ropi/picture alliance

Hata hivyo  mkutano huo huenda ukagubikwa na suala la hatua ya kihistoria iliyochukuliwa jana na rais wa Marekani Joe Biden ya kutogombea muhula wa pili madarakani.

Mkutano huo unafanyika katika kiwingu cha  wasiwasi kote barani Ulaya kuhusu uwezekano wa Donald Trump kurudi tena madarakani nchini Marekani.

Soma pia:Rais Zelensky asaini makubaliano ya kiusalama na EU

Mawaziri hao  wanatarajiwa kujadili kuhusu msaada wa Umoja wa Ulaya kwa Ukraine pamoja na uharibifu uliofanywa katika miundo mbinu yake ya nishati, ambayo imekuwa ikishambuliwa na Urusi. Waziri wa mambo ya kigeni wa Ukraine Dmytro Kuleba pia anatarajiwa kujiunga na mkutano huo kwa njia ya video.

Mazungumzo ya Brussels pia yanatarajiwa kujadili  hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza kufuatia vita vya Israel na Hamas,pamoja na mivutano inayoongezeka katika eneo la mpaka kati ya Israel na Lebanon.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW