1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

EU yaidhinisha msaada zaidi wa kijeshi kwa Ukraine

24 Juni 2024

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya wameidhinisha msaada wa kijeshi wa dola bilioni 1.4 kwa ajili ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4hRYE
Bendera ya Umoja wa Ulaya
Bendera ya Umoja wa Ulaya Picha: Shakh Aivazov/AP Photo/picture alliance

Kifurushi hicho kwa mara ya kwanza kitafadhiliwa na mapato ya mali ya Benki kuu ya Urusi iliyozuiliwa.

Mkuu wa sera za kigeni wa Ulaya Josep Borrell amesema fedha hizo zinatakiwa kupelekwa Ukraine mara moja na kuepuka kizuizi chochote kabla ya kuidhinishwa katika mkutano wa mawaziri wa Ulaya huko Luxembourg.

Idhini hii inatolewa kama nyongeza ya kuipiga jeki Kyiv katikati ya upinzani unaoendelea wa Hungary kuelekea misaada mingine kutoka kwenye mfuko usio wa kibajeti wa Umoja wa Ulaya, EPF wenye thamani ya zaidi ya yuro bilioni 6.