1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mataifa ya Afrika Mashariki yaandika historia AFCON

27 Septemba 2023

Nchi tatu za Afrika Mashariki - Kenya, Uganda na Tanzania - zimeandika historia leo baada ya kuchaguliwa kwa pamoja kuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON ya mwaka 2027.

https://p.dw.com/p/4WsvV
AFCON Finale Senegal vs Ägypten Sadio Mane
Mchezaji wa timu ya taifa ya Senegal Sadio Mane akiwa na kombe baada ya kutwaa ushindi wa michuano ya mataifa ya Afrika Picha: Charly Triballeau/Getty Images/AFP

Uamuzi huo uliosubiriwa kwa shauku na mashabiki wa soka wa kanda hiyo umetangazwa leo mchana na Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF, baada ya kamati yake utendaji kupiga kura mjini Cairo. 

Mataifa hayo matatu yaAfrika Mashariki yalikuwa yanachuana na Misri, Botswana, Algeria na Senegal. 

Soma pia:Cameroon yaifunga Burundi, Ufaransa yachapwa na Ujerumani

Hiyo itakuwa mara ya kwanza kwa nchi hizo kuandaa tamasha hilo kubwa la kabumbu barani Afrika tangu Ethiopia ilipokuwa mwenyeji wa michuano ya AFCON mwaka 1976. 

Mbali ya nchi hizo tatu,CAF pia imeiteuwa Morocco kuandaa michuano ya AFCON ya mwaka 2025.