1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cameroon yaifunga Burundi, Ufaransa yachapwa na Ujerumani

13 Septemba 2023

Timu ya Cameroon imefunga usiku wa jana Burundi mabao 3-0, na hivyo kufuzu kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika hapo mwakani nchini Ivory Coast.

https://p.dw.com/p/4WGVe
FIFA Fussball-Weltmeisterschaft Katar 2022 | Gruppe G | Kamerun - Brasilien
Picha: Dylan Martinez/REUTERS

Ushindi huu wa Cameroon umeitoa timu hiyo katika nafasi ya mwisho hadi ya kwanza katika kundi C na jumla ya alama 7, ushindi ulioinufaisha pia timu ya Namibia inayofuzu kwa jumla ya alama 5. Cameroon ni nchi ya pili kwa mafanikio katika michuano ya Afcon ikiwa tayari imeshinda taji hilo mara tano.

Na katika mechi nyingine,

Fußball | Freundschaftsspiel Deutschland - Frankreich | Thomas Müller
Mchezaji wa Ujerumani Thomas Müller akishangilia baada ya kupachika bao:12.09.2023Picha: Martin Meissner/AP Photo/picture alliance

Ujerumani ambayo itakuwa mwenyeji hapo mwakani wa michuano ya kuwania Kombe la Mataifa ya Ulaya imeifunga Ufaransa mabao 2-1 mjini Dortmund katika mechi ya kirafiki. Kocha wa muda Rudi Völler ndiye aliyekiongoza kikosi cha Ujerumani na kuamua kumrejesha uwanjani Thomas Mueller ambaye alipachika bao la kwanza katika dakika nne za mwanzo. Kocha Hansi Flick  alifutwa kazi siku ya Jumapili baada ya kuwa na matokeo duni na timu hiyo ya taifa ya Ujerumani.