1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya mitandaoni kwa wagombea urais Kongo

16 Desemba 2023

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kumekuwa na ongezeko la mashambulizi ya mitandaoni ikiwa zimesalia siku chache kwa raia wa taifa hilo kushiriki uchaguzi wa rais wa Desemba 20.

https://p.dw.com/p/4aEoB
Kandidaten für die Präsidentenwahl in der Demokratischen Republik Kongo Moise Katumbi
Mgombea urais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Moise Katumbi Picha: Nicolas Maeterlinck/picture alliance

Baadhi ya shutuma zinasambazwa mitandaoni kwa nia ya kuharibu sifa za wapinzani wanaoshiriki kinyang'anyiro cha urais kuelekea uchaguzi  mkuu unaotaraji kufanyika hivi karibuni nchini Jamuhuri ya Kidemikrasia ya Kongo, ni madai yanayoenezwa juu ya kuwepo wagombea feki ama kuwataja baadhi ya wagombea kuwa ni raia wa kigeni. Madai hayo yanatumika kama silaha ili kuwamaliza baadhi ya wagombea wa upinzani.

Mwandishi wa habari wa tovuti inayochunguza ukweli kuhusu Kongo (Kongo Check), Marien Nzikou-Massala amechapisha jumbe zinazolalamikia kuwa kuna baadhi ya wagombea ni wazambia, na wengine kutajwa ni wagiriki, zingine zikienda mbali na kueleza kuwa mgombea fulani ameoa mwanamke mwenye asili ya Rwanda. Mwandishi huyo ameongeza kusema, katika kipindi cha uchaguzi mjini Kinshasa, taarifa potofu zinaenea kwa kasi zaidi kuliko taarifa sahihi.

Haya yanajiri wakati  upande wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wakikabiliana na ongezeko la ghasia na vitendo vya uhalifu dhidi ya kundi la waasi wa M23 wanaodaiwa kuungwa mkono na nchi jirani ya Rwanda.

Kuongezeka kwa mashambulizi ya mitandaoni

DR Kongo Kinshasa | Präsident Felix Tshisekedi und Denis Mukwege | Treffen
Mgombea uras katika Jamhuri ya Kongo,Denis MukwegePicha: Giscard Kusema/Präsidentschaftspresse der DR Kongo

Tangu kuanza kwa kampeni ya uchaguzi wa Desemba 20, mashambulizi ya mtandaoni yamekuwa yawalenga zaidi wapinzani wanaoaminika kuwa ni tishio zaidi kwa Rais Felix Tshisekedi, ambaye anawania muhula wa pili.

Mamia ya watumiaji wa mtandao wanawashutumu wagombea wa upinzani akiwemo mfanyabiashara tajiri, Moise Katumbi na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Denis Mukwege, kuwa ni wageni waliopewa uraia wa Kongo ila wana asili ya aidha Rwanda, Zambia, Burundi au Uganda.

Wanamitandao pia wametumia kama ushahidi, picha na video zilizorekodiwa mwaka 2018 katika kongamano lililoandaliwa na taasisi ya Afrika, zikiwaonesha rais wa Rwanda Paul Kagame akiwa na Katumbi na wanaelezea kuwa wawili hao walikutana hivi karibuni.

Shutuma kuhusu Katumbi na uraia wake

Shutuma dhidi ya Katumbi mtandaoni zinazohoji juu ya asili yake kama ni Muitaliano, Mgiriki ama Mzambia zimezuka kutokana a historia ya mzazi wake wa kiume ambae alikua Myahudi wa Sephardic aliezaliwa Rhodes, wakati ambapo kisiwa cha Ugiriki kikitawaliwa na Italia, na baadae akahamia mpakani mwa Zambia na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kusini Mashariki.

Nae Mukwege ambae elimu yake ameipata Burundi na barani Ulaya, wanamitandao wanaeleza kuwa kwa asilimia zote mgombea huyo ni Mrundi na uraia alionao wa Kongo ni batili.

Shutuma hizo ambazo hazijathibitishwa zimekua zikikuzwa zaidi kwenye mitandao, pia zimekua zikiripotiwa na vyombo vya habari na hata kutumika na wagombea wengine wakati wa mikutano yao ya kampeni.

Namna uadui dhidi ya Rwanda unavyoathiri uchaguzi mashariki mwa Kongo

Demokratische Republik Kongo | Junior und Jonathan
Vijana Junior na Jonathan wakufuatilia jambo kuhusu uchaguzi mtandaoniPicha: Paul Lorgerie/DW

Kwa mujibu wa mtafiti wa masuala ya kisiasa kutoka kituo cha utafiti cha mjini Kinshasa Ebuteli, Ithiel Batumike kwenye majimbo yaliyo Mashariki, uadui wa Umma dhidi ya Rwanda na Burundi unaochochewa na mizozo ya mara kwa mara ya kivita.

Mtafiti huyo ametolea mfano Kivu Kaskazini, ambapo amesema iwapo mtu atasema mgombea fulani anashirikiana na Rwanda, basi hilo litapelekea kupunguza umaarufu alionao na imani juu ya wapiga kura wake pia itapotea.

Batumike pia ameonya juu ya kile alichoeleza kuwa ''uvumi kuhusu utaifa na asili ya wagombea'' wakati wa maandalizi ya uchaguzi ni hatari kwa umoja wa kitaifa na hudhoofisha mshikamano wa nchi.

Wasiwasi wa jumiya ya kimataifa juu ya ongezeko la vurugu

Ongezeko la mvutao huo limechochea pia Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa, kuonesha hali ya wasiwasi juu ya ogezeko la hatari ya makabiliano ya kijeshi baina ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda.

Kwa upande wake mtaalamu wa masuala ya siasa Jean- Luc Kong Mbalu amesema,  huo ni mkakati unaotumiwa na wanasiasa kudhoofisha wapizani, ambapo ameeleza kwa Kongo kuendesha mijadala ya uchaguzi inayolenga miradi ifanywayo na wagombea ni aghalabu, mara nyingi hutumia uasili wao kuwasema ikizingatiwa suala la utaifa nchini humo limewekwa katika katiba.

Mataalamu huyo ameonya juu ya hali hiyo ya hatari aliyoiita ''roho ya kujitenga'' ambayo amesema iwapo itakita mizizi kwa watu huenda ikageuka na kuwa chuki dhidi ya wageni.

Sheria hiyo iliyoanzishwa mwaka 2003, kufutia mazungumzo ambayo yaliyopelekea kuungana tena kwa nchi hiyo, baada ya muongo wa vita, iliamuru kuwa suala la kuwa na uraia wa nchi mbili nchini humo ni kinyume cha sheria, kwa kuhofia kuingiza mamluki katika jeshi la Kongo. 

Soma zaidi:Kuelekea kura DRC, vijana watamani ajira

Mgombea urais Noel Tshiani aliomba mahakama ibatilishe ugombea wa Moise Katumbi, huku akieleza kuwa mgombea huyo alikua na uraia wa Italia, ombi ambalo mahakama ya katiba ililitupilia mbali.

Kwa upande wake msimamizi wa mitandao ya kijamii wa asasi iitwayo "Search for Common Ground, Christian Cirhigiri" amesema, kuna mgawanyiko wa utambulisho kati ya Wakongo wa Mashariki na Magharibi na wagombea wengi wanaoandamwa mitandaoni ni wale wanaotokea Mashariki.  

Chanzo: AFP