1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekebu 3 za wakimbizi

20 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDJt

MADRID:

Marekebu 3 zaidi zikisheheni wahamiaji wasio halali wa kiafrika zimewasili kwenye visiwa vya Canary leo hii,zikipakia jumla ya abiria 1.000 mnamo siku tatu zilizopita.Vituo vya mapokezi vimesheheni mno na serikali ya Spain imebidi kuwasafirisha kwa ndege wakimbizi hao hadi bara ya Spain huku ikijaribu kusaka njia ya kuwarejesha makwao.

Waziri mkuu wa Spain, Jose KLuis Rodriguez ,amearifu kwamba, waziri wake wa ulinzi atafunga safari kwenda Senegal hapo kesho.