1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yatuma manuri za kijeshi karibu na mwambao wa Lebanon

Kalyango Siraj29 Februari 2008

Manuari yake ya USS Cole iliwahi kushamabuliwa nchini Yemen

https://p.dw.com/p/DFgy

Marekani inatuma manuari zake za kijeshi katika bahari ya Mediterranean karibu na Lebanon katika kile kinachoonekana kama kuonyesha nguvu wakati wa mvutano wa kisiasa nchini Lebanon.

Mvutano wa kisiasa katika nchi ya Lebanon pamoja na kuisota kidole nchi jirani ya Syria kuwa, kwa njia moja inahusika na kile uvurugaji wa masuala ya siasa katika nchi ya Lebanon,umeifanya Marekani kulazimika kuchukua hatua ya kutuma manuari za kijeshi katika eneo hilo.

Manuari zinazozungumzwa hapa ni tatu. Hatua hiyo inaochukuliwa kama kutiwa na wasiwasi kutokana na hali tete ya kisiasa katika eneo hilo.Lakini mkuu wa vikosi vya Marekani Admiral Michael Mullen amewaambia maripota kuwa -hatua hii isichukuliwe kama ya kutisha ama kutokana na tukio lolote la katika nchi moja katika eneo hilo tete.

Afisa mmoja wa kijeshi ambae hakutaka jina lake kutambuliwa amesema kuwa miongoni mwa manuari ambazo zinatumwa mashariki mwa bahari ya Mediterrenea karibu na Lebanon ni ile inayoitwa Missile Destroyer USS Cole ikifuatiwa na nyingine mbili zinazobeba mafuta.

Manuari ya USS Cole iliwahi kulengwa na kundi la Al Qaida oktoba 2000 katika bandari ya Aden-Yemen,ambapo wanamaji 17 wa Marekani waliuliwa.

Msemaji wa wizara ya Ulinzi ya Marekani amesema kuwa manuari hiyo kwa sasa iko katika maeneo ya mashariki mwa bahari ya Mediterrenean.Hata hivyo hakutoa maelezo zaidi kuhusu eneo hasa manuari hiyo ilipo.

Msemaji wa Ikulu ya White House-Gordon Johndroe alipoulizwa ikiwa rais George W Bush ndie alitoa amri hiyo, amejibu kuwa rais anatilia maanani hali ya ilivyo kwa sasa nchini Lebanon na kila mara hujadilia suala hilo kila mara na ujumbe wa uslama wa kitaifa.

Lebanon imeingia miezi minne ikiwa haina rais- na haionekani ikiwa mzozo huo unaweza ukatatuliwa hivi karibuni.Jambo hilo limeleta wasiwasi wa mgawanyiko huo unaoendelea kuwa unawaweza ukazusha mapigano ya wao kwa wao.

Viongozi wa nchi za kiarabu wamejaribu kuziba pengo liliopo kati ya ushirika tawala unaoungwa mkono na nchi za magharibi na upande wa upinzani unaoungwa mkono na Syria pamoja na Iran.

Lakini wachambuzi wa mambo wanasema kuwa juhudi hizo huenda haizitazaa matunda hadi pale mkutano wa nchi za kiarabu utakao fanyika mwezi ujao.

Mapigano kati y makundi yanayopinzana yaliyotokea juzi katika barabara za mjini Beirut,yalishababisha nchi kadha katika eneo la Ghuba na pia nchi za magharibi kuwashauri raia wake kujizuia kushawishika kwenda Lebanon.

Waziri wa Mashauri ya kigeni wa Saudi Arabia-mwanawa -ufalme Saud al-Faisal,mapema mwezi huu, alionya kuwa Lebabon inakaribia kujitosa katika vita vya ndani.

Hali hiyo iliongezewa chumvi, wakati kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah ,kuapa kuanzisha vita dhidi ya Israel,akiilaumu kwa kuhusika katika mauaji ya kamanda wa ngazi ya juu wa Hezbollah,yaliyotokea Febuari 12 mjini Damascus.

Syria inalaumiwa kwa kumuua waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafiq Hariri mwaka wa 2005.Hata hivyo Syria, ambayo wakati huo ilikuwa na majeshi yake huko, ilikanusha kuhusika na miezi miwili baadae ikaondoa majeshi yake kutoka Lebanon.Inasemekana baado inaushawishi mkubwa nchini humo ikiunga mkono washia walio na msimamo mkali.