1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yatoa wito wa uwazi kwa uchaguzi wa Kongo

22 Desemba 2023

Marekani imetoa mwito wa kuwepo uwazi katika uchaguzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya zoezi la upigaji kura kuongezwa muda hadi siku ya pili kufuatia changamoto ya usafirishaji wa vifaa.

https://p.dw.com/p/4aTQq
DR Kongo Wahltag
Picha: Paul Lorgerie/DW

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa wizara ya mambo ya nje imeeleza kuwa "Marekani haitokaa kimya iwapo kutatokea makosa ambayo huenda yakahujumu mchakato huo wa kidemokrasia."Washington imerejelea mwito wake wa kuwepo uwazi kutoka kwa tume ya uchaguzi ya CENI ili "kujenga imani katika mchakato huo."Rais Felix Tshisekedianasakamuhula wa pili madarakani katika taifa hilo kubwa zaidi kusini mwa Jangwa la Sahara. Zoezi la upigaji kura lilianza siku ya Jumatano japo liliongezwa muda hadi jana Alhamisi katika baadhi ya maeneo kutokana na kuchelewa kuanza kwa zoezi hilo huku matokeo ya awali ya urais yakitarajiwa kuanza kutolewa hii leo.