1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yatangaza ushirikiano na nchi 50 kukabili magonjwa

16 Aprili 2024

Utawala wa rais wa Marekani Joe Biden umetangaza mpango mpya wa ushirikiano na nchi 50, kukabili magonjwa ya kuambukiza.

https://p.dw.com/p/4erHc
Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Andrew Harnik/Getty Images

Lengo ni kuzuia miripuko ya magonjwa kama ya virusi vya corona vilivyovuruga kwa ghafla maisha ya kawaida kote ulimwenguni mwaka 2020.

Kulingana na afisa wa ngazi ya juu katika utawala wa Biden, Marekani itashirikiana na nchi hizo kutengeneza mifumo imara ya uchunguzi, majaribio, mawasiliano na utayari wa kukabili miripuko kama hiyo kwenye mataifa husika.

Soma pia:WHO yatarajia makubaliano ya "kihistoria"

Afisa aliyezungumza na waandishi wa habari amesema Kongo ni miongoni mwa nchi hizo ambazo mipango hiyo imeshaanza