1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Homa kali yawakumba watoto wengi nchini Ujerumani

9 Desemba 2022

Taasisi ya Robert Koch inayoshughulikia magonjwa ya mlipuko nchini Ujerumani inasema zaidi ya watu milioni saba wameathiriwa na aina tofauti za maambukizi katika kipindi cha mwezi mmoja tu.

https://p.dw.com/p/4KjKE
Atemwegserkrankung
Picha: H.Wiedl/picture-alliance/ZB

Kulingana na taasisi Robert Koch, aina mbili za virusi vya magonjwa hayo vinasambaa barani kote Ulaya na hasa Ujerumani. Kirusi cha kwanza kinasababisha mafua, na kingine, ambacho ni hatari zaidi kwa watoto wachanga na wa umri mdogo, kinashambulia mfumo wa upumuaji.

Matokeo yake, katika baadhi ya maeneo ya Ujerumani, hakuna tena vitanda vilivyo wazi katika vituo vya afya kwa ajili ya watoto wa umri huo.

Wakati wa kilele cha mlipuko wa Covid-19, maambukizi ya  mafua yalipungua sana kwa sababu katika kipindi hicho watu wengi walizingatia sana kanuni za usafi,  kama kunawa mikono mara kwa mara, kuvaa barakoa na kuacha nafasi kati ya mtu mmoja na mwingine. Na Ilikuwa vigumu zaidi kwa virusi vya kila aina kuenea haraka.

Changamoto za corona 

Kinga za watoto wadogo na wachanga  hazikukukabiliana na virusi vya mafua
Kinga za watoto wadogo na wachanga  hazikukukabiliana na virusi vya mafuaPicha: Michael Bihlmayer/CHROMORANGE/picture allianc

Mwaka huu, kutokana na kupungua kwa uangalifu na tahadhari, virusi vya mafua husambaa kwa urahisi zaidi. Kwa hiyo wagonjwa ni wengi kuliko kawaida. Watoto wengi ambao hawakuambukizwa miaka miwili iliyopita wameambukizwa msimu huu wa baridi. 

Kigezo kingine ni kwamba watoto walio wagonjwa wakati huu hawakupata fursa ya kujenga kinga ya mwili dhidi ya virusi vinavyosababisha mafua. Wakati kingamwili hizi zinaruhusu mwili kupambana na virusi na kuilinda dhidi ya vimelea vya magonjwa. Kwa sababu ya sheria za usafi wa Covid, kinga za watoto wadogo na wachanga  hazikukukabiliana na virusi vya mafua.

Kwa hivyo sasa maambukizi yanazidi kupanda zaidi. Taasisi Robert Koch tayari imeonya kuwa maambukizi hayaonekani kumalizika, na kuwa, Idadi bado inaweza kuongezeka duniani kote ingawa Umoja wa Ulaya hivi karibuni uliidhinisha dawa ya kutibu matatizo ya kupumua iliyotengenezwa na makampuni ya AstraZeneca na Sanofi.

Ujerumani sio pekee inayohusika. Ufaransa, kwa mfano, tayari iliandaa mpango wa dharura mapema Novemba kukabiliana na janga la ugonjwa huo wa kupumua miongoni mwa watoto wachanga na wadogo.