1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaitaka Kongo kutatua 'mzozo wa uchaguzi' kwa amani

1 Januari 2024

Marekani imetowa wito wa kutatuliwa kwa amani na uwazi mizozo yoyote ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya Rais Felix Tshisekedi kutangazwa mshindi wa uchaguzi katika taifa la Afrika ya Kati

https://p.dw.com/p/4alTY
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo- Felix Tshisekedi wakati wa mkutano nchini Ubelgiji
Rais wa Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo- Felix TshisekediPicha: Pool Vlad Vanderkelen/Belga/picture alliance

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani amesema kuwa Washington inafuatilia mchakato huo kwa ''karibu'' bila ya kutoa mara moja pongezi zake kwa Tshisekedi.

Msemaji huyo ameendelea kusema kuwa "mizozo yoyote ya uchaguzi inapaswa kutatuliwa kwa amani na kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Kongo'' na akatoa wito kwa mamlaka husika ''kuhakikisha malalamiko yoyote yanashughulikiwa kwa haki na uwazi."

Soma pia:Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilifanya uchaguzi wa urais mnamo Disemba 20, ingawa upinzani unaupinga kwa madai ya udanganyifu

Matokeo ya awali yanaonesha kuwa Tshisekedi ameshinda uchaguzi huo kwa asilimia 73 ya kura, ambazo tayari viongozi wa upinzani wamezipuuza na kuzitaja kuwa ni "za uongo."

Mahakama ya kikatiba ya Kongo inatarajiwa kuthibitisha matokeo hayo ya awali mnamo Januari 10.