1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Marekani yasema Kim atarajia kukutana na Putin

5 Septemba 2023

Marekani inasema kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un anatarajiakukutana na rais wa Urusi Vladimir Putin kuzunumzia juu ya kuipelekea silaha Urusi kwa ajili ya vita vyake nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4VxNy
Russland Nordkorea Gipfel in Wladiwostok | Kim Jong Un und Putin
Picha: Kremlin Pool/Russian Look/picture alliance

Marekani imesema kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un anatarajia kukutana na rais wa Urusi Vladimir Putin kujadili kuipelekea silaha kwa ajili ya vita vyake nchini Ukraine.

Tangazo hilo limetolewa baada ya ikulu ya Marekani kutahadharisha wiki iliyopita kwamba Urusi kwa njia ya siri ilikuwa tayari ikifanya mazungumzo na Korea Kaskazini kupata silaha kadhaa na mahitaji mengine kwa juhudi zake za vita.

Kwa mujibu wa gazeti la Marekani la The New York Times Kim huenda akasafiri mwezi huu kwenda Vladivostok mji wa wa pwani ya bahari ya Pasifiki ambao hauko mbali sana na Urusi, kukutana na rais Putin.

Gazeti hilo aidha limeripoti kuwa Kim jJong Unhuenda hata akasafiri kwenda mjini Moscow, lakini hilo halina uhakika. Urusi na Korea Kaskazini hazijasema lolote kuthibitisha mkutano kati ya viongozi wao.