1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Marekani yaionya Korea Kaskazini juu ya kuiuzia silaha Urusi

31 Agosti 2023

Marekani imeionya Korea Kaskazini dhidi ya kuiuzia silaha Urusi huku mvutano kati ya Pyongyang na Washington ukiendelea.

https://p.dw.com/p/4VmGI
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akisalimiana na Rais wa Urusi Vladimir Putin
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akisalimiana na Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Alexander Zemlianichenko/AP Photo/picture alliance

Utawala wa Rais Joe Biden umesema kuwa, Urusi na Korea Kaskazini zinajadiliana juu ya makubaliano ya silaha.

Msemaji wa baraza la usalama wa kitaifa wa Marekani John Kirby amesema waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu hivi karibuni alisafiri hadi Korea Kaskazini ili kuishawishi nchi hiyo kuiuzia Urusi silaha.

Kirby ameongeza kuwa, tangu ziara hiyo, Rais wa Urusi Vladimir Putin na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wamekuwa wakiandikiana barua, na kuahidi kuongeza ushirikiano kati yao.

Marekani imekuwa ikiwaonya wapinzani wake ikiwemo China juu ya kuisaidia Urusi katika vita vyake nchini Ukraine.