1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaipa Ukraine silaha za Iran ilizozikamata

5 Oktoba 2023

Marekani imeipa Ukraine risasi zipatazo milioni 1.1 ambazo ilizitwaa kutoka kwenye meli iliyokuwa inazisafirisha zana hizo kutoka Iran ili kuzipeleka kwa waasi wa nchini Yemen.

https://p.dw.com/p/4X9Lb
Kosovo | Beschlagnahmte Waffen in Mitrovica
Picha: Vudi Xhymshiti/VX/picture alliance

Kituo kikuu cha kijeshi cha Marekani (Centcom) kinachosimamia operesheni za kijeshi katika Mashariki ya Kati kimesema zana hizo zilikamatwa na jeshi la majini la Marekani mnamo mwezi Desemba mwaka uliopita wakati zikiwa njiani kupelekwa Yemen.

Nchi za magharibi zinazoisaidia Ukraine hivi majuzi zilitanabahisha kwamba zinangàngàna katika kutengeneza zana kwenda sambamba na kiwango kinachotumiwa na Ukraine.

Marekani imesema silaha hizo zilizotoka Iran, zilipelekwa Ukraine mapema wiki hii. Serikali ya Marekani ilipata umiliki wa silaha hizo mwezi Julai kutokana na mchakato unaoruhusu kutwaa mali ikiwa mmiliki wa mali husika anajihusisha na harakati za kihalifu.