1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaihimiza Kongo kutatua mizozo ya uchaguzi

2 Januari 2024

Marekani imetoa wito wa kutatuliwa kwa amani na uwazi mizozo yoyote ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya Rais Felix Tshisekedi kutashinda kwa kupata asilimia 73 ya kura.

https://p.dw.com/p/4ao81
Felix Tshisekedi
Rais wa Kongo Felix TshisekediPicha: Arsene Mpiana/AFP/Getty Images

Marekani imetoa wito wa kutatuliwa kwa amani na uwazi mizozo yoyote ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya Rais Felix Tshisekedi kutashinda kwa kupata asilimia 73 ya kura.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani ametoa wito kwa serikali ya Kongo kuhakikisha kwamba malalamiko yote yanashughulikiwa kwa haki na uwazi. Mahakama ya Katiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inatarajiwa kuthibitisha matokeo hayo mnamo Januari 10.

Moise Katumbi mfanyabiashara tajiri, mmiliki wa klabu ya soka na gavana wa zamani wa mkoa  wa Katanga anashika nafasi ya pili wa kwa kupata takriban asilimia 18. Katumbi na wagombea wengine wanane wa upinzani wametia saini tamko la kupinga matokeo ya uchaguzi na wataka urudiwe tena.

Zaidi ya watu milioni 40 kati ya wakazi milioni 100 nchini Kongo walijiandikisha kupiga kura iliyofanyika Desemba 20 kwa ajili ya kumchagua rais, pamoja na wabunge wa kitaifa na wa kikanda na madiwani wa manispaa.