1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani, NATO waishinikiza Hungary kuiidhinisha Sweden

5 Februari 2024

Marekani na washirika wengine wa Jumuiya ya kujihami ya NATO wanazidi kuishinikiza Hungary kuiidhinisha Sweden kujiunga na muungano huo wa kijeshi.

https://p.dw.com/p/4c4DD
 Brüssel | NATO
Barua rasmi za Sweden na Finland kujiunga na NATOPicha: NATO

Marekani na washirika wengine wa Jumuiya ya kujihami ya NATO wanazidi kuishinikiza Hungary kuiidhinisha Sweden kujiunga na muungano huo wa kijeshi.

Soma: Bunge la Uturuki laidhinisha Sweden kujiunga na NATO

Mjumbe wa Marekani mjini Budapest pamoja na mabalozi kutoka nchi kadhaa nyingine washirika wa jumuiya hiyo akiwemo wa Denmark na Poland wamehudhuria kikao cha bunge la Hungury leo Jumatatu katika tukio la ghafla la kuishinikiza nchi hiyo kuikubalia Sweden kujiunga na mfungamano huo wa kijeshi.

Hadi sasa Hungary ni nchi pekee mwanachama wa NATO ambayo haijaidhinisha  ombi la uanachama wa Sweden,hatua ambayo imeuharibu uhusiano wake na Marekani na kuibuwa wasiwasi miongoni mwa washirika wake.

Upinzani nchini Hungary ulioitisha kikao hicho cha dharura cha bunge,kuhusu suala la Sweden,unasema waziri mkuu Viktor Orban anataka kuegemea zaidi upande wa Urusi huku akivunja ushirikiano na jumuiya ya NATO.

Wabunge wa chama cha Orban wamesusia kikao hicho cha leo.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW