1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sweden kutojadiliana na Hungary kuhusu NATO

26 Januari 2024

Waziri Mkuu wa Sweden, Ulf Kristersson, amesema hawatajadiliana na Hungary juu ya ombi lake la kutaka kujiunga na Muungano wa Kijeshi wa NATO, ingawa ndiyo mwanachama pekee ambaye bado hajaidhinisha ombi la Sweden.

https://p.dw.com/p/4bj3a
Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson.
Waziri Mkuu wa Sweden Ulf Kristersson.Picha: Henrik Montgomery/TT/IMAGO

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg, ameeleza imani yake kuwa bunge la Hungary litaidhinisha ombi la Sweden mwishoni mwa mwezi huu.

Mawaziri wakuu wa Sweden na Hungary watakutana wiki ijayo mjini Brussels, lakini Kristersson amesema Sweden haitatoa ahadi zozote mpya kuhusu NATO wakati wa mkutano huo.

Soma zaidi: Bunge la Uturuki laidhinisha Sweden kujiunga na NATO

Sweden na Finland zilituma maombi ya kujiunga na jumuiya hiyo ya kujihami mwaka 2022 baada ya Urusi kuivamia Ukraine.

Hata hivyo, uwanachama wao ulipingwa na Uturuki na Hungary na kuziacha nchi hizo katika njia panda.

Washirika wa NATO wanaiona Sweden kama kiungo muhimu katika usalama eneo la Baltiki.