1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Venezuela zabadilishana wafungwa

21 Desemba 2023

Marekani na Venezuela zimebadilishana wafungwa. Serikali ya Rais Joe Biden imemuwachilia huru mshirika wa Rais wa Venezuela Nicolas Maduro.

https://p.dw.com/p/4aQoU
Joe Biden wa Marekani
Rais wa Marekani Joe Biden Picha: Yuri Gripas/ZUMA Wire/IMAGO

Katika makubaliano hayo ikulu ya Marekani imesema imemwachia Alex Saab mfanyabiashara wa Colombia na mshirika wa karibu wa rais Maduro.

Saab anatuhumiwa na Marekani kwa utakatishaji fedha kwa niaba ya serikali ya Venezuela.

Kwa upande wake Venezuela imemachia mtoro Leonard Francis aliyehusishwa na kashfa kubwa kabisa ya rushwa ya jeshi la wanamaji la Marekani.

Maafisa wa Marekani wamesema nchi hiyo inatumai kwamba hatua zilizofikiwa kati ya nchi hiyo mbili hasimu zitafungua milango ya kuendelea na mazungumzo na kwamba Venezuela itafuata njia ya kidemokrasia katika siku zijazo.