1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na mjadala kuhusu silaha za kuangamiza:

25 Januari 2004
https://p.dw.com/p/CFhD
WASHINGTON: Nchini Marekani umezidi kutiwa makali ule mjadala kuhusu shutuma iwapo Iraq ikidhibiti silaha za kuangamiza. Mgombea wa kiti cha Rais wa chama cha kidemokrasi John Edwards ametoa mwito kuwa iundwe halmashauri maalumu ya kuchunguza shutuma hizo. Halmashauri hiyo itabidi ichunguze iwapo Rais George W. Bush amelihadaa bunge kabla ya kuanzisha vita vya Iraq, alisema mgombea Edwards mkoani New Hampshire. Serikali ya Marekani imeitumia shutuma hiyo ya silaha za kuangamiza kama sababu yake kubwa kabisa ya kuanzisha vita dhidi ya Iraq. Sasa kwa mara ya kwanza Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Colin Powell amekiri kuwa ana shaka zake iwapo Iraq ikidhibiti silaha za kuangamiza wakati vilipoanza vita. Kwa maoni ya mkaguzi wa silaha wa zamani wa Marekani David Kay, kabla ya kuanza vita Iraq ilipeleka Syria sehemu ya silaha zake, lakini haikudhihirika aina ya silaha zilizohamishwa, alisema Bwana Kay.