1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Kim Jong Un anapanga kukutana na Putin

5 Septemba 2023

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un anapanga kumtembelea rais Vladimir Putin wa Urusi kujadili uwezekano wa kuipatia Moscow silaha kwa ajili ya vita nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4VyNg
Russland Nordkorea Gipfel in Wladiwostok | Kim Jong Un und Putin
Picha: Korean Central News Agency/Korea News Service/AP Photo/picture alliance

Hayo yameelezwa na afisa mmoja wa ngazi ya juu wa serikali ya Marekani ambaye amesema majadiliano ya kupeana silaha kati ya Urusi na Korea Kaskazini yamepiga hatua na pande hizo mbili zinataka kuyasogeza mbele kupitia mkutano baina ya viongozi wao wakuu.

Kim atarajiwa kukutana na Putin nchini Urusi

Kulingana na gazeti la New York Times, Kim huenda atafanya ziara hiyo ya nadra nje ya nchi baadae mwezi huu akitumia treni hadi kwenda mji wa mwambao wa bahari ya Pasifiki upande wa Urusi wa Vladivostok, kwa mkutano wake na rais Putin. 

Kwa miezi kadhaa sasa Marekani imekuwa ikitoa hadhari kwamba Urusi inafanya mazungumzo ya siri na Korea Kaskazini kujipatia silaha na mahitaji mengine ili kuendeleza vita nchini Ukraine.