1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yazuka baina ya jeshi la Kongo na waasi wa M23

Benjamnin Kasembe28 Machi 2022

Kumeshuhudiwa mapambano makali asubuhi ya leo jumatatu katika vijiji kadhaa vya mkoa wa Rutshuru jimboni Kivu ya Kaskazini baina ya jeshi na waasi wa M23.

https://p.dw.com/p/497q4
Kongo I FDLR Rebellen
Picha: Dai Kurokawa/dpa/picture alliance

Maelfu ya wakimbizi kutoka katika baadhi ya vijiji vya kando na milima ya chanzu na runyoni wameonekana tangu asubuhi ya leo juma tatu wakivuka mpaka kuelekea nchi jirani ya uganda kufuatia mapigano  makali yanayo endelea hadi muda huu kati ya jeshi la Congo na kundi la waasi wa M23 .

Vyanzo kutoka asasi zairaia vimethibitisha kutekwa upya kwa milima ya runyoni na chanzu wilayani rutshuru ambayo  walikuwa wanatumia kama ngome yao kuu chini ya kamanda sultani makenga ,mwaka wa 2012 habari ambazo bado jeshi la congo kuthibitisha. 

Kuzuka upya mapigano haya kati ya pande zote hizo mbili kumewatia hofu wanaharakati haki za bianadamu ambao wameitaka kamati ya kimataifa kuingilia kati mzozo huo unao weza kuyaathiri mataifa jirani kama anavyo fafanua KUSUDI mapendo wa kundi la CADH.

Soma pia→Rwanda na DRC zachunguza kurudi kwa wapiganaji wa M23

Machafuko yasiokwisha

Kongo 2012 - Soldaten der M23-Rebellenbewegung
Picha: Imago/Kyodo News

Hadi tunapo enda hewani na matangazo haya, jeshi la congo FARDC laendelea kurusha mabomu kuelekea maeneo ya milima inayo kaliwa sasa na kundi hilo la waasi wa M23 ambao mara kadhaa wamekuwa wakiishutumu serikali ya congo kwa kuvunja mapatano kati yao ambayo ilikuwa ni njia pekee yakuleta amani upande wa mashariki.

Kurejea kwa kundi la M23 kunaripotiwa wakati serikali ya rais wa DRC Felix Tshisekedi inapambana na waasi kutoka uganda wa ADF katika wilaya ya beni na ituri operesheni ambazo hadi sasa hazija leta mafanikio makubwa.