1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mapigano yaripotiwa kupungua mjini Khartoum, Sudan

30 Mei 2023

Mapigano yanaelezwa kupungua katika mji mkuu wa Sudan, Khartom leo hii ingawa wakazi wanasema yaliendelea kusikika katika baadhi ya maeneo, baada ya pande mbili hasimu kukubaliana kuongeza muda wa usitishaji mapigano.

https://p.dw.com/p/4Rypw
Sudan, Khartoum | zerstörte und geplünderte Tankstelle
Picha: AFP/Getty Images

Wakazi waliripoti mapigano Alasiri ya leo karibu na eneo la kambi ya jeshi iliyoko kusini mwa Khartoum. Lakini pia saa kadhaa kabla ya muda wa nyongeza ya usitishaji mapigano kutiwa saini walitoa taarifa ya mapigano makali katika miji mitatu ya Khartoum, Omdurman na Bahri.

Soma pia: Mkataba wa usitishaji mapigano Sudan warefushwa kwa siku tano zaidi

Vita hivyo vimesababisha karibu watu milioni 1.4 kukimbia makazi yao, wakiwemo zaidi ya 350,000 ambao wamevuka mpaka kuingia katika matiafa jirani.