1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

M23 waudhibiti mji wa kimkakati Kitshanga

23 Oktoba 2023

Waasi wa M23 wameudhibiti upya mji wa kimkakati wa Kitshanga wilayani Masisi baada ya mapigano makali kati yao na wanamgambo wanaojiita "Muungano wa Vijana Wazalendo."

https://p.dw.com/p/4Xty3
Wapiganaji wa M23.
Wapiganaji wa M23. Picha: Guerchom Ndebo/AFP

Wiki iliyopita, mji huo wa Kitshanga ulikuwa umedhibitiwa na Vijana hao wazalendo, lakini waliukimbia tangu jana asubui kufuatia shambulizi kali la waasi wa M23 dhidi ya ngome zao. 

Vyanzo mbalimbali vimesema waasi wa M23 walivurumisha mabomu kuelekea mji huo ulioko umbali wa kilomita 80 kutoka mji wa Goma, na kuwajeruhi baadhi ya wakaazi na wengine walipewa hifadhi katika kambi ya kijeshi ya Umoja wa Mataifa kwenye eneo hilo.

Soma pia:Mapigano mapya yazuka mashariki ya Congo

Kulingana na raia, waasi wa M23 wameendelea kushika doria hadi leo asubuhi, bila ya upinzani wowote kutoka vikosi vya Umoja wa Mataifa na Kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki.