1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine: Kiev yakabiliwa na usiku mwingine wa mashambulizi

Zainab Aziz Mhariri:Saumu Njama
27 Februari 2022

Mji mkuu wa Ukraine, Kiev wakabiliwa na shambulio makali ya Urusi. Wakati huo huo, mataifa ya Magharibi yanapanga kuziondoa baadhi za Urusi kutoka kwenye mfumo wa fedha wa kimataifa (SWIFT).

https://p.dw.com/p/47fAG
Ukraine Invasion
Picha: Emilio Morenatti/AP/picture alliance

Taarifa ya jeshi la Ukraine imesema kuwa wanajeshi hao wa Urusi pia wanakabiliwa na upinzani mkubwa ikiwa pamoja na vikosi hivyo vya Ukraine kuzuia shambulio la Urusi karibu na mji wa Kharkiv ulio kaskazini, mashariki mwa Ukraine.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Rais wa Ukraine Volodymyr ZelenskyPicha: Ukrainian President's Office/ZUMA Press/picture alliance

Ofisi ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy imesema kumetokea mlipuko kwenye bomba la gesi, kusini mwa mji mkuu wa Kiev mapema Jumapili. Amri ya kutotoka nje imewekwa katika mji huo mkuu wa hadi kesho Jumatatu.

Soma:Makabiliano makali yaendelea nje kidogo ya Kyiv

Balozi wa Ukraine nchini Ujerumani Andrij Melnyk ameelezea furaha yake kutokana na uamuzi wa Ujerumani wa kupeleka silaha nchini Ukraine. Balozi Andrij Melnyk ameliambia shirika la habari la Ujerumani (dpa) kuwa hatua hiyo ni ya kihistoria.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi, UNHCR, limesema takriban watu 150,000 wamekimbia mapigano kutoka Ukraine na kuingia katika mataifa jirani.

Wakimbizi kutoka Ukraine waingia nchini Poland
Wakimbizi kutoka Ukraine waingia nchini PolandPicha: Darek Delmanowicz/PAP/dpa/picture alliance

Msemaji wa UNHCR, Shabia Mantoo, ameeleza kuwa idadi hiyo inaoongezeka kila dakika na shirika hilo la kuwashughulikia wakimbizi, linakadiria kuwa huenda takriban watu milioni 4 wa Ukraine wakaikimbia nchi hiyo iwapo hali itaendelea kuwa mbaya. Mantoo amesema watu wengi wanakimbilia katika nchi jirani za Poland, Moldova, Hungary, Romania na Slovakia na Belarus.

Wakati huo huo, nchi za Magharibi zinapanga kuzitoa benki fulani za Urusi kutoka kwenye mfumo wa benki wa SWIFT. Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema hatua hiyo itahakikisha kwamba benki zitasitisha ushirikiano na Urusi katika mfumo wa kimataifa ili kutatiza maswala ya kifedha ya Urusi kimataifa.Rais wa Ukraine ahofia mji mkuu, Kiev kushambuliwa na majeshi ya Urusi awataka wananchi waulinde

Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen
Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der LeyenPicha: Dursun Aydemir/AA/picture alliance

Ujerumani, Umoja Ulaya, Marekani na Uingereza zimetangaza vikwazo hivyo vipya dhidi ya Urusi ingawa awali Ujerumani ilipinga hatua hiyo ikisema inaweza pia kuudhuru uchumi wa dunia.

Soma:

Kwa upande wake Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litakutana leo Jumapili kwa mara ya nne ndani ya wiki moja. Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya pia watashiriki kwenye mkutano huo kwa njia ya video kujadili msaada zaidi kwa Ukraine na hatua zaidi za adhabu dhidi ya Urusi.

Vyanzo: RTRE/DPA/AP/https://p.dw.com/p/47f2S