1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mzigo haubebeki

Admin.WagnerD31 Agosti 2016

Mwaka mmoja uliopita Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alitoa kauli ambayo sasa imekuwa maarufu ,aliposema "tutaweza," yaani kuwahudumia wakimbizi. Na jee atafanikiwa.?

https://p.dw.com/p/1JsPI
Picha: picture-alliance/dpa/T. Carmus

Maoni yanatautiana. Wapo wanaosema ataweza. Lakini katika maoni yake Mhariri Mkuu wa DW Alexander Kudascheff anasema jukumu hilo litamzidi kimo, Bibi Merkel. Kansela Merkel aliifungua milango yote na kuwakaribisha maalfu kwa maalfu ya wakimbizi nchini Ujerumani.

Lakini hitawezekana, kuyatimiza aliyoahidi kwa sababu haijulikani ni nini hasa kinapangwa kutimizwa, kuwaangalia tu wakimbizi hao au kuwatangamanisha na jamii. Mimi nasema hatutaweza kwa sababu hatujui ni nini tunachokitaka kukifanikisha. Hututafanikiwa kwa sababu hatujui ni nini tunaweza kusema.

Miaka 25 baada ya nchi mbili za kijerumani kuungana tena Wajerumani wengi wanasema, kwa kweli bado hatujaunganika. Sababu ni kwamba tunalizingatia jukumu kitaaluma, badala ya kuliangalia kitamaduni, na ndiyo sababu kwamba tunapaswa kujifunza kuziona tofauti.

Hata hivyo badala yake tunafikiri kwamba wakimbizi wanakuja kujaza mapengo yanayotokana na kupungua kwa idadi ya watu nchini.

Nasema hatutaweza kwa sababu,hutujui kwamba tunawageuza wakimbizi kuwa wahamiaji.Lakini watu hao ni wahafidhina na waumini wakubwa wa dini kuliko jamii yetu ya kisasa kwa wastani.

Ujerumani si nchi ya wahamiaji

Hatutaweza kwa sababu pia hatujui juhudi inayohitajika,katika kuwafanya watu wanaotoka kwenye tamaduni nyingine wajione kuwa wako nyumbani. Sisi tunayo mazingira tunayoyaita kuwa ni kwetu, lakini wahamiaji hawaonyeshi hisia kwamba hapa ni kwao, kilugha,kitamaduni na kisiasa.

Mwandishi wa maoni Alexander Kudascheff
Mwandishi wa maoni Alexander Kudascheff

Ujerumani siyo nchi ya wahamiaji, na ndiyo sababu, aghalabu,hatutumii busara tunapowapokea watu hao, badala yake tunaamini tunaweza kuwashughulikia kwa kufuata hisia tu. Hatutafinikiwa kwa sababu hatuwachagui wahamiaji hao bali tunawachukua tu.

Mbali na hayo uhusiano wetu na taifa letu wenyewe ni butu na ndio sababu kwamba hatuakisi mfano wa uhakika,kwa usemi mwingine hatuna mwongozo kwa sababu pana mfarakano nyumbani mwetu. Licha ya maelezo yote yanayotolewa bado hatujawa tayari kuwa na utangamano wa tamaduni nyingi kama jinsi mara nyingi Rais wetu anavyojaribu kusawiri.

Hatutaweza kwa sababu jukumu hilo linahitaji muda mrefu sana wa zaidi ya marika matatu, na tuliifumbia macho changamoto hiyo.

Sababu nyingine ni kwamba tumewapokea wakimbizi wengi kutoka Syria na Afghanistan ambao hawataweza kwenda sambamba na kasi ya nchi hiii iliyoendelea sana kiviwanda- nchi yenye ufanisi wa juu. Na pia wahamiaji wengi hawataweza kufikia viwango vya ufanisi vya nchini Ujerumani.

La mno kabisa linalotoka katika kauli ya "tutaweza"ni kusema tu kwamba tunayo matumaini ya kufanikiwa. Lakini inapasa kutambua kwamba katika hulka ya Mjerumani mna hofu zaidi kuliko matumaini . Na siku moja tutasema, tungeliweza kufanikiwa, hata ikiwa tumeshindwa .

Mwandishi:Kudascheff, Alexander

Mfasiri:Mtullya abdu.

Mhariri: