1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bwana mmoja akamatwa baada ya mwili wa mtoto kutupwa mtoni

8 Oktoba 2023

Bwana mmoja huko magharibi mwa Ujerumani ametiwa mbaroni baada ya binti yake wa umri wa miaka mitatu kufa kwa kufungiwa katika chumba cha chini ya jengo la ghorofa na baadaye kuutupa mwili wake katika mto mdogo.

https://p.dw.com/p/4XGXY
Deutschland Migranten in Forst an der deutsch-polischen Grenze
Picha: Lisi Niesner/REUTERS

Taarifa ya polisi na waendesha mashtaka ilisema bwana huyo, Mjerumani wa umri wa miaka 40, Ijumaa alikwenda katika kituo cha polisi cha mji wake wa asili, Dinslaken, na kuwaambia maafisa kuwa binti yake amekufa na kutokana na kuzidiwa uzito mwili wake aliamua kuutupa katika mto ulio karibu na mji wa Oberhausen.Wachunguzi walisema wanaamini kuwa bwana huyo alikuwa amemfunga msichana huyo kwenye chumba cha chini cha jengo alilokuwa akiishi kwa siku chache, kwa kile kinachoonekana kama kumpa funzo.Waokozi waliweza kuupata mwili wa binti huyo Ijumaa na uchunguzi wa awali ulibaini kuwa masaa machache kabla ya kifo chake alitapika hadi kifo.Hata hivyo, mwili wake haukuwa na dalili ya majeraha ya kipigo.