1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani tayari kurudisha mavufu Afrika Mashariki

19 Januari 2023

Mamlaka ya Makumbusho ya mjini Berlin iko tayari kuyarudisha mamia ya mafuvu ya vichwa kutoka Afrika Mashariki. Hatua hii inakuja baada ya kufanya utafiti kwa miaka kadhaa na kutambua asili yake.

https://p.dw.com/p/4MQ3m
Niederlande I Völkermord Prozess vor Gericht in Den Haag
Picha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Utafiti huo ulifanyiwa mafuvu zaidi ya elfu moja ambapo 904 kati ya hayo huenda yakapelekwa Rwanda, 202 Tanzania na 22 nchini Kenya.

Watafiti hawakuweza kutambua asili ya mafuvu mengine saba. Kulingana na Wakfu wa Urithi wa Kitamaduni wa Prussia, idadi kubwa ya mafuvu hayo yalitolewa makaburini ila baadhi yalitoka sehemu zilizokuwa zikitumiwa kufanya mauaji na baadhi yalitokana na mauaji yaliyofanywa na Wajerumani kipindi cha ukoloni.