1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamilioni ya dola kutolewa ili kukabiliana na hewa ukaa

4 Septemba 2023

Nchi kadhaa zimeahidi kutowa mamilioni ya dola kwaajili ya juhudi za kuimarisha mfuko wa kusimamia shughuli za kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa kufikia mwaka 2030.

https://p.dw.com/p/4VwnB
Kenia Nairobi | Africa Climate Summit 2023 | William Ruto, Präsident, Kenia
Picha: Monicah Mwangi/REUTERS

Ahadi hizo zimetolewa katika mkutano wa kihistoria wa kilele kuhusu mazingira wa viongozi wa Kiafrika,uliofunguliwa leo na rais wa Kenya William Ruto. 

Umoja wa Falme za Kiarabu umeahidi kutowa dola milioni 450 kwaajili ya kusaidia miradi ya masoko ya Kiafrika ya upunguzaji viwango vya uzalishaji hewa ukaa,(ACMI). 

Soma pia:Viongozi wa Afrika wakutana kujadili masuala ya mazingira

Mradi wa Masoko hayo ulianzishwa nchini Misri kufuatia mkutano wa kilele wa COP 27 mwaka jana.

Mkuatano wa kilele wa siku tatu wa Nairobi,kwa mujibu wa waandalizi,unalenga kulitangaza  bara la Afrika kama kituo cha uwekezaji wa miradi ya  kimazingira badala ya kutazamwa  kama muhanga wa mafuriko na njaa.

 


 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW