1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UAE yamualika Assad katika mkutano wa mazingira wa COP 28

15 Mei 2023

Umoja wa Falme za Kiarabu, UAE, umemualika Rais wa Syria Bashar al-Assad katika mkutano wa mazingira wa COP 28 utaokaofanyika ndani ya umoja huo mwisho wa mwaka huu.

https://p.dw.com/p/4RNVG
VAE Abu Dhabi | Herrscher Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan
Picha: Jon Gambrell/AP/picture alliance

Shirika la habari la serikali ya Syria, SANA, limeripoti kuwa mwaliko huo umetolewa na Rais wa Umoja huo Sheikh Mohammed bin Zayed. Ubalozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu mjini Damascus pia umeandika ujumbe sawa na huo kupitia akaunti yake ya mtandao wa Twitter.

Mataifa mengine ya Kiarabu yameanza kulegeza misimamo yao mikali dhidi ya Syria baada ya kumtenga Assad kwa zaidi ya muongo mmoja kufuatia hatua ya serikali yake kutumia nguvu kupita kiasi kupambana na waandamanaji na baadaye kugeuka kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Mahusiano ya kidiplomasia kati ya Syria na mataifa ya Kiarabu yalifufuka upya kufuatia tetemeko la ardhi la Februari 6 lililoikumba Syria na Uturuki.