1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mamia ya wahamiaji wa Afrika wawasili visiwa vya Canary

4 Oktoba 2023

Mamia ya wahamiaji kutoka mataifa ya Afrika wamewasili kwenye visiwa vya Canary nchini Uhispania wakitumia boti ya mbao kufanya safari hiyo hatari ya kuvuka bahari.

https://p.dw.com/p/4X6UC
Wahamiaji nchini Tunisia
Wahamiaji nchini TunisiaPicha: Hasan Mrad/IMAGESLIVE via ZUMA Press Wire/dpa/picture alliance

Waokoaji wamesema chombo hicho kilikuwa kimesheheni idadi kubwa ya watu wapatao 271 waliowasili kwenye eneo la El Hierro magharibi mwa visiwa vya Canary.

Asasi ya Msalaba mwekundu iliyowahudhumia wahamiaji hao wamesema idadi hiyo ndiyo kubwa zaidi kubwa kuwahi kupokelewa miaka ya karibuni ya watu waliosafiri kwa kutumia boti moja.

Mwaka 2008 kundi la wahamiaji 234 waliingia visiwa vya Carnay wakitumia chombo kimoja.

Mamlaka za visiwa hivyo zinasema katika muda wa saa 24 zilizopita jumla ya wahamiaji 726 ikiwemo wanawake na watoto wamefika visiwani humo kutumia vyombo sita tofauti visivyo na viwango vyovyote vya usalama.

Visiwa vya Canary vinavyoundwa na fungu la visiwa saba limekuwa eneo kuu linalotumiwa na wahamiaji kuifikia Uhispania huku wengine wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterrania kuingia eneo la bara ya Uhispania.