1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Serikali ya Mali yaandaa mazungumzo ya amani

27 Januari 2024

Serikali ya Mali imeunda kamati ya kuandaa mazungumzo ya amani ya kitaifa baada ya kutupilia mbali makubaliano muhimu ya amani ya mwaka 2015.

https://p.dw.com/p/4bkYD
Kiongozi wa kijeshi wa Mali Choguel Kokalla Maïga
Mkuu wa serikali ya kijeshi ya Mali Choguel Kokalla Maïga amesema wanaandaa mazungumzo kwa ajili ya kusaka amani ya kudumuPicha: Adam Diko

Mkuu wa serikali ya kijeshi, Choguel Kokalla Maiga amesema kwenye mkanda wa video uliochapishwa kwenye mitandao ya kijamii jana Ijumaa kwamba hawatarudia tena kutafuta suluhu kutoka nje.

Algeria ilikuwa mpatanishi mkuu katika juhudi za kurejesha amani kaskazini mwa Mali, katika makubaliano yaliyosainiwa mjini Algiers mwaka 2015 kati ya serikali ya Mali na makundi yenye silaha ya kabila la Tuareg.

Makubaliano hayo hata hivyo yalianza kuvunjwa mwaka jana baada ya kuzuka mapigano kati ya wanaotaka kujitenga na jeshi la serikali mnamo mwezi Agosti baada ya miaka minane ya utulivu, wakati pande zote zikihangaika kuziba pengo lililoachwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa walioondoka.