1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Algeria yasikitishwa na Mali kusitisha makubaliano na Tuareg

26 Januari 2024

Algeria imeonesha kusikitishwa na uamuzi wa utawala wa kijeshi wa Mali wa kusitisha makubaliano ya amani ya mwaka 2015 na waasi wa Tuareg wanaotaka kujitenga.

https://p.dw.com/p/4bjEx
Wapiganaji wa kundi la Tuareg nchini Mali.
Wapiganaji wa kundi la Tuareg nchini Mali.Picha: Souleymane Ag Anara/AFP

Algeria inayopakana na Mali katika eneo la urefu wa kilomita 1,300, imesema kusitishwa kwa makubaliano hayo kunaweza kulihatarisha eneo hilo wakati ambapo kuna ongezeko la vitisho vya kigaidi.

Soma zaidi: Mali yasitisha makubaliano na Watuareg

Algeria ilikuwa mpatanishi mkuu katika juhudi za kurejesha amani kaskazini mwa Mali kufuatia makubaliano yaliyotiwa saini katika mji mkuu wake Algiers mwaka 2025 kati ya serikali ya Mali na waasi wa Tuareg mwaka 2015.

Makubaliano hayo yalichukuliwa kuwa muhimu katika kuleta utulivu nchini Mali, taifa maskini na liliso na bandari la Afrika Magharibi.