1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMalaysia

Malaysia yampunguzia adhabu Waziri Mkuu wa zamani Najib

Sylvia Mwehozi
2 Februari 2024

Bodi ya taifa ya kutoa misamaha Malaysia imetangaza kumpunguzia adhabu ya kifungo jela waziri mkuu wa zamani Najib Razak aliyehukumiwa kwa ubadhirifu na utakatishaji wa fedha katika kashfa ya mabilioni ya dola.

https://p.dw.com/p/4bxWo
Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Najib Razak
Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Najib RazakPicha: AP Photo/picture alliance

Najib Razak ambaye alikuwa akitumikia kifungo cha miaka 12 gerezani ataachiwa huru Agosti mwaka 2028, huku faini aliyopewa nayo ikipunguzwa kufikia dola milioni 10 kutoka milioni 50.

Bodi hiyo inayoongozwa na Mfalme wa Malaysia haikutoa sababu za kupunguzwa kwa adhabu hiyo.

Najib alitiwa hatiani kwa ufisadi unaohusishwa na mpango wa maendeleo wa Malaysia 1MDB, ambapo inakadiriwa kwamba dola bilioni 4.5 ziliibwa na nyingine zaidi ya bilioni moja zilihamishiwa katika akaunti zilizounganishwa na waziri mkuu huyo wa zamani.