1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Najib Razak arejeshwa jela

Josephat Charo
6 Novemba 2023

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Najib Razak amerejeshwa gerezani kutoka hospitali alikokuwa amelazwa. Razak aliugua ugonjwa wa Covid 19 lakini vipimo vimeonyesha hana tena ugonjwa huo.

https://p.dw.com/p/4YR1E
Malaysia | Najib Razak
Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Najib RazakPicha: Vincent Thian/AP Photo/picture alliance

Waziri Mkuu wa zamani wa Malaysia Najib Razak ametolewa hospitali na kurejeshwa gerezani baada ya kupatikana hana tena ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya corona. Taarifa hiyo imetolewa jana Jumapili na msemaji wake.

Najib mwenye mri wa miaka 70, anatumikia kifungo cha miaka 12 jela baada ya kutiwa hatiani kwa ufisadi na utakatishaji fedha katika kesi inayohusiana na kashfa ya mabilioni ya dola. Alilazwa hospitali wiki iliyopita alipopimwa na kupatikana na ugonjwa huo.

(reuters)