1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUswisi

Makubaliano ya NATO ya Uswidi yanaweza kufikiwa

5 Juni 2023

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg amesema makubaliano juu ya Sweden kujiunga na muungano huo yanaweza kufikiwa kwa wakati kwa ajili ya mkutano wa kilele mwezi ujao nchini Lithuania.

https://p.dw.com/p/4SCCP
Schweden | NATO-Generalsekretär Jens Stoltenberg
Picha: Jonas Ekstromer/TT News Agency/AP/picture alliance

Stoltenberg ameyasema hayo baada ya kukutana mjini Istanbul na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ambaye ataendeleza muhula wake wa uongozi kwa miongo miwili baada ya kushinda uchaguzi.

Soma pia:NATO yajadili hakikisho la usalama wa Ukraine baada ya vita 

Katibu mkuu huyo wa NATO amesema pia kuwa maafisa kutoka Uturuki, Sweden na Finland watakutana kwa mazungumzo baadaye mwezi huu ili kujaribu kuondoa pingamizi kutoka kwa Uturuki na Hungary ambazo zimeichelewesha Sweden kujiunga na NATO.