1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliojeruhiwa kwa bunduki waongezeka Marekani

31 Machi 2023

Utafiti mpya nchini Marekani unaonesha pale ambapo kunakuwa na tukio la kuuwawa kwa mtu mmoja nchini humo, kunakadiriwa kuwapo pia manusura mmoja au wawili huku kwa kiwango kikubwa kuwepo mtu aliyejeruhiwa vibaya sana

https://p.dw.com/p/4PWlx
USA | Proteste | March for Our Lives
Picha: REUTERS

Wataalamu wanasema ni vyema kutambua athari za vurugu zitokanazo na matumizi ya bunduki katika jamii. Aidha utafiti huo unaonesha hali ya kipindi cha hivi karibuni inayoonesha idadi kubwa ya walijeruhiwa kwa risasi katika kipindi cha janga la UVIKO-19, wakati ambapo kulikuwa na idadi kubwa ya watu waliofyatuliana risasi au baadhi kujifyatulia.

Chapisho la Taasisi ya Kudhibiti na Kuzuia Magonjya ya Marekani CDC limesema katika kipindi cha miaka miwili ya kwanza ya janga hilo, idadi ya watu waliojeruhiwa kwa risasi iliongezeka kufikia asilimia 40, ikilinganishwa na 2019.

2022 Majeruhi walipungua ingawa kiwango kilibaki kuwa cha juu

Katika kipindi cha mwaka 2022, majeruhi wa risasi walipungua ingawa bado walisalia kuwa katika asilimia 20 ikiwa ni kiwango cha juu ikilinganishwa kabla ya janga

USA | Proteste | March for Our Lives
Maandamano ya kupinga matumizi ya bunduki Brooklyn Picha: REUTERS

Walijeruhiwa kwa bunduki waliongezeka kwa wake na waume katika muda wa miaka mitatu iliyopita miaka, wakati ongezeko kubwa lilitokea kati ya watoto chini ya miaka 15, ikiwa ni sehemu ya tatizo katika matumizi holela ya silaha nchini Marekani.

Wataalamu wanasema utafiti wa kujeruhiwa kwa bunduki wa CDC, ambao unatumia takwimu kutoka hospitali idara za dharura, husaidia kutoa picha ya kina zaidi ya vurugu zenye kuhusisha bunduki nchini Marekani kuliko kuweka ulinganifu wa kipimo cha mauaji na kujiua.

Hospitali ni sehemu njema ya kutambua athari za bunduki Marekani

Mtafiti mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Harvard Catherine Barber anasema hospitali ni sehemu nzuri ya kuweza kupata utambuzi wa nani hasa aliyejeruhiwa kwa kupigwa risasi, lini na wapi. Mmoja kati ya waandishi wa utafiti huo mpya, Thomas Simon alisema matokeo ya utafiti wa CDC ni baada ya kuhusisha zaidi ya hospitali 2,200 za Marekani, idara za dharura.

Kimsingi utafiti unaonesha idadi ya wagojwa ambao walijeruhiwa kwa risasi mahospitalini imeongezeka kwa watu elfu 50 zaidi ikilinganishwa na mwaka 2019 na kadhalika zaidi ya elfu 72 kwa mwaka 2020. Lakini pia kwa kuwa zaidi ya robo ya vitengo vya dharura vya Marekani havijahusishwa katika utafiti huo inawezekana kuwa idadi kamili ikawa kubwa kuliko hii inayowekwa hadharini kwa wakati huu.

Soma zaidi:Biden alaani shambulizi la shule huko Nashville

Watafiti wanaaamini kuwa miongoni mwa sababi zenye kuchangia janga hilo la matumizi ya bunduki kuongezeka ni pamoja na hali ya kuongezeka kwa manunuzi ya bunduki, zinatumika zaidi kwa matumizi ya nyumbani kwa kuwa zipo katika familia pamoja na shida ya afya ya akili ambayo inachangiwa zaidi na baadhi kutengwa na jamii pamoja na ugumu wa maisha.

Chanzo: AP