1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Mahakama Pakistan yamfungulia mashtaka mengine Imran Khan

23 Oktoba 2023

Mahakama nchini Pakistan imemfungulia mashtaka waziri mkuu wa zamani, Imran Khan, kwa madai ya kuvujisha maudhui ya mawasiliano ya siri ya kidiplomasia.

https://p.dw.com/p/4Xtw2
Waziri wa zamani wa Pakistan Imran Khan
Waziri wa zamani wa Pakistan Imran KhanPicha: Akhtar Soomro/REUTERS

 Madai hayo yanafunguliwa kukiwa tayari na mkururo wa kesi nyengine kwa kiongozi huyo aliye jela kabla ya uchaguzi wa taifa hilo.

Jaji Mohamed Zulqarnain amesema Khan pamoja na aliyekuwa waziri wake wa mambo ya kigeniwatalazimika kufunguliwa mashitaka kwa kuvujisha siri hizo za taifa kwenye mkutano wa hadhara.

Soma pia:Nawaz Sharif arejea Pakistan baada ya miaka minne

Mahakama maalumu itakuwa ikirekodi matamko ya mashahidi baadaye wiki hii, hii ikiwa ni kulingana na mahakama baada ya kesi ya awali ndani ya gereza anakozuiliwa Khan.
 
Wanasiasa hao wote wawili wamekanusha kutofanya kosa hilo. Ikiwa watakutwa na kosa, wanaweza kukabiliwa na kifungo cha miaka miwili jela na kupigwa marufuku kushiriki siasa.