1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Khan kuzuiwa kwa wiki mbili zaidi Pakistan

30 Agosti 2023

Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan ataendelea kuzuiliwa rumande katika jela moja lenye ulinzi mkali kwa karibu wiki mbili zaidi licha ya kupewa dhamana.

https://p.dw.com/p/4VkNU
Pakistan | Protest gegen die Verhaftung von Imran Khan
Picha: Asif Hassan/AFP/Getty Images

Kulingana na wakili wa Khan, mahakama imetoa uamuzi huo baada ya kikao kifupi cha kusikiliza kesi katika jela la Attock mashariki mwa mkoa wa Punjab. Wakili huyo anasema kikao chengine cha kusikilizwa kwa kesi hiyo kitakuwa Septemba 2.

Uamuzi huu ni pigo kwa Khan na kikosi chake cha mawakili kwa kuwa mahakama moja Islamabad jana ilisimamisha kifungo chake cha miaka mitatu kwa madai ya ufisadi.

Wakili wake mwengine Salman Safdar amewaambia waandishi wa habari kwamba ameukatia rufaa uamuzi huo wa mahakama wa kumzuia rumande. Khan anazuiliwa kutokana na kesi ya uvujishwaji wa nyaraka za siri inayomkabili.