1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

India: Korti yafuta msamaha wa wanaume waliobaka na kuua

8 Januari 2024

Mahakama ya Juu nchini India leo imeufuta msamaha uliotolewa kwa wanaume 11 wa kihindu ambao walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kumbaka kwa zamu mwanamke mmoja muislamu na kuwauwa ndugu zake.

https://p.dw.com/p/4ayJ2
Mkuu wa tume ya wanawake Swati Maliwal akiwa pamoja na wanaharakati wengine kulalamikia ongezeko la matukio ya ubakaji na uhalifu dhidi ya wanawake
Mkuu wa tume ya wanawake Swati Maliwal akiwa pamoja na wanaharakati wengine kulalamikia ongezeko la matukio ya ubakaji na uhalifu dhidi ya wanawakePicha: Mayank Makhija/NurPhoto/picture alliance

Uhalifu huo ulimefanyika wakati wa ghasia za kidini zilizolitikisa jimbo la Gujarat zaidi ya miongo miwili iliyopita.

Kwenye mkasa huo wa mwaka 2002 uliotokea katikati ya mapambano baina ya jamii za wahindu na waislamu, wanaume hao walimbaka kwa zamu Bilkis Bano, aliyekuwa wakati huo mjamzito na kisha kuwauwa ndugu zake 7 ikiwemo mtoto wake wa miaka mitatu.

Soma pia:  Watu 41 walionasa ardhini kwa waki mbili India wako mbioni kuokolewa

Walitiwa hatiani mnamo mwaka 2008 lakini waliachiwa huru mwaka 2022 baada ya jela walimokuwa wakitumia kifungo cha maisha kupendekeza iwapatiwe msamaha kwa msingi kwamba walionesha tabia njema.

Uamuzi huo ulizusha hasira na ukosoaji kote nchini India na watu wa kadhaa walifungua shauri la kuupinga mahakamani.

Katika uamuzi wake wa leo, Mahakama ya Juu imeamuru wanaume hao wajisalimishe mara moja gerezani ndani ya muda wa wiki mbili zinazokuja.