1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Mahakama India yakataa kuhalalisha ndoa za jinsia moja

18 Oktoba 2023

Mahakama ya Juu ya India imekataa kuhalalisha la ndoa za jinsia moja lakini ikasema nchi hiyo ina wajibu wa kuyatambua mahusiano kati yao na kuwalinda kutokana na ubaguzi.

https://p.dw.com/p/4Xdm4
Indien | Der indische Premierminister Narendra Modi
Picha: Adnan Abidi/REUTERS

Akisoma hukumu yake, Jaji Mkuu D. Y. Chandrachud alisema ni jukumu la bunge kutoa muongozo wa sheria ya ndoa na haki msingi ya ndoa kwa wanandoa wa jinsia moja haijaainishwa na kulindwa na katiba ya India chini ya sheria ya sasa.

Serikali ya Waziri Mkuu Narendra Modi imekuwa ikipinga hatua za kuhalalisha rasmi ndoa za jinsia moja katika kipindi cha miaka mitano tangu mahakama ya juu kabisa ilipofuta sheria zinazopiga marufuku kufanya mapenzi  kati ya watu wa jinsia moja za enzi ya ukoloni.