1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mafunzo ya matumizi ya ndege F-16 yaanza Ukraine

20 Agosti 2023

Waziri wa Ulinzi wa Ukraine Oleksiy Reznikov amesema wanajeshi wa Ukraine wameanza kufunzwa namna ya kutumia ndege za kisasa za kivita chapa F-16.

https://p.dw.com/p/4VN2h
F-16 Kampfjet der Niederländischen Luftwaffe
Picha: Joerg Waterstraat/SULUPRESS/picture alliance

Mafunzo hayo yatachukua miezi sita au zaidi kukamilika. Matamshi ya Reznikov yamekuja siku mbili baada ya afisa mmoja wa Marekani kusema ndege hizo zitapelekwa Ukraine baada ya marubani wake kukamilisha mafunzo hayo. 

Urusi yaonya mipango ya kuipatia Ukraine ndege za kivita

Afisa huyo alisema Marekani iko tayari kutuma ndege hizo kutoka Denmark na Uholanzi baada ya mafunzo hayo ili kuisadia Ukraine kujilinda dhidi ya uvamizi wa Urusi

Ukraine inahitaji ndege hizo za kisasa kukabiliana na uvamizi wa angani kutoka Urusi iliyoanza uvamizi wake mwezi Februari mwaka 2022.