1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Urusi yaonya mipango ya kuipatia Ukraine ndege za kivita

28 Mei 2023

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi Sergei Lavrov ameyaonya mataifa ya magharibi dhidi ya makubaliano yao ya kuipatia Ukraine ndege za kisasa za kivita chapa F16.

https://p.dw.com/p/4Ruif
Sergei Lavrov
Waziri wa Mambo ya kigeni wa Urusi, Sergei Lavrov Picha: Vyacheslav Prokofyev/TASS/IMAGO

Mwanadiplomasia huyo ametoa matamshi hayo katika sehemu ya mahojiano yake na kituo kimoja cha televisheni nchini Urusi yayolirushwa kupitia mitandao ya kijamii. Lavrov amesema nchi za magharibi "zinacheza na moto" na kukosoa kile amekitaja kuwa jaribio la "kuidhoofisha Urusi" linalofanywa na Marekani, Uingereza na washirika wake wa Ulaya.

Dhamira ya kuipatia Ukraine ndege zinazotumia teknolojia mamboleo, chapa F16, ilitangazwa wakati wa mkutano wa kilele wa kundi la G7 uliomalizika wiki iliyopita nchini Japan.

Hata hivyo viongozi wa nchi za magharibi wamesema mara kadhaa kuwa silaha wanazoipatia serikali ya mjini Kyiv hazipaswi kutumika kuilenga Urusi nje ya mipaka ya Ukraine.