1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Watu waukimbia mji mkuu wa Haiti unaokumbwa na machafuko

16 Agosti 2023

Maelfu ya wakaazi wanaondoka katika kitongoji kinachokumbwa na machafuko ya magenge ya uhalifu katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince.

https://p.dw.com/p/4VFBz
Maafisa wa polisi wa Haiti katika oparesheni dhidi ya magenge ya wahalifu
Maafisa wa polisi wa Haiti katika oparesheni dhidi ya magenge ya wahalifuPicha: Odelyn Joseph/AP Photo/picture alliance

Maafisa wa Idara ya Ulinzi wa Raia nchini Haiti wamesema mpaka sasa inakadiriwa kuwa watu 3,120 wamelikimbia eneo hilo, na wengine wanatarajiwa kuwafuata.

Kitongoji hicho hushambuliwa mara kwa mara na genge linaloongozwa na Renel Destina, almaarufu Ti Lapli, ambaye anasakwa na maafisa wa Marekani kwa kuwateka nyara raia wa Marekani.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitolea mwito jamii ya kimataifa kupeleka kikosi maalumu cha kimataifa kitakachojumuisha wanajeshi na polisi nchini Haiti kukabiliana na magenge ya uhalifu yenye silaha za kisasa.

Guterres ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa kuna mambo mawili makubwa ya kufanywa ambayo ni msaada wa vifaa kwa vikosi vya kimataifa na polisi ya Haiti pamoja na kuimarisha ujumbe wake uliopo nchini humo.