1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Guterres atoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuisaidia Haiti

2 Julai 2023

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, ametaka juhudi kubwa za kimataifa zifanyike kusaidia polisi nchini Haiti kukabiliana na changamoto katika kupambana na magenge ya wahalifu yaliyokithiri nchini humo.

https://p.dw.com/p/4TJpW
Kenia l UN Generalsekretär Antonio Guterres in Nairobi
Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Guterres amesema hayo  alipofanya ziara yake ya kwanza kama mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuangazia vurugu na machafuko nchini humo. Kwenye ziara hiyo, Guterres alikutana na kufanya mazungumzo na waziri mkuu Ariel Henry, viongozi wa asasi za kijamii, wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na vyama vya siasa. 

Guteress asema lazima Haiti iwekwe kwenye ramani ya kisiasa ya kimataifa

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa aliwaambia wanahabari kwamba ni lazima waiweke Haiti kwenye ramani ya kisiasa ya kimataifa, na kuyafanya mahangaiko ya watu wa Haiti yapewe kipaumbele na jumuiya ya kimataifa. Guterres amesema alikutana na raia wa Haiti na kuona uchovu wa watu ambao wamekuwa wakikabiliwa na msururu wa migogoro na hali mbaya ya maisha kwa muda mrefu.