1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Polisi wa Sudan wawafukuza raia waliojihifadhi shuleni

9 Novemba 2023

Polisi nchini Sudan wamewaondoa kwa nguvu mamia ya raia waliokuwa wamejihifadhi katika shule moja katika jimbo la mashariki la Gedaref.

https://p.dw.com/p/4Yahd
Moshi ukifuka katika mji wa Khartoum wakati wa makabiliano kati ya majeshi ya Sudan dhidi ya wanamgambo wa RSF
Moshi ukifuka katika mji wa Khartoum wakati wa makabiliano kati ya majeshi ya Sudan dhidi ya wanamgambo wa RSFPicha: Ahmed Satti/AA/picture alliance

Polisi inawafukuza raia hao wakati jeshi la nchi hiyo na wapiganaji wa kikosi cha RSF wakiendelea kupambana mjini Khartoum.

Mkazi mmoja Amal Hussein amesema alishuhudia magari ya polisi yakiizingira shule hiyo na kusikia watu wakipiga mayowe. Mkazi mwingine aliyekimbia mapigano huko Khartoum Hussein Gomaa amesema polisi waliwataka kuondoka shuleni hapo kufuatia maagizo ya gavana na kuwafyatulia gesi ya machozi.

Gomaa ameliambia shirika la habari la AFP kwamba watu wapatao 770 walikuwa wamejihifadhi kwenye eneo hilo baada ya kukimbia mapigano.

Amesema hawajui sababu hasa za kuondolewa na kusema kwa sasa wako nje na hawana mahali pa kwenda.

Gedaref kwa sasa inawahifadhi watu 273,000 waliokimbia makazi yao kutokana na mzozo na Umoja wa Mataifa umesema maelfu wanaishi kwenye makambi ya muda yenye upungufu mkubwa wa maji safi na huduma za afya.