1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mapigano yaendelea Sudan licha ya kurejea kwa mazungumzo

30 Oktoba 2023

Wakuu wa kijeshi wanaohasimiana nchini Sudan wameanza tena kufanya mazungumzo nchini Saudi Arabia.

https://p.dw.com/p/4YBsr
Zaidi ya watu elfu 9 wameuwawa katika miezi sita ya mapigano huko Sudan.
Zaidi ya watu elfu 9 wameuwawa katika miezi sita ya mapigano huko Sudan.Picha: Umit Bektas/REUTERS

Lakini licha ya kuanza kwa mazungumzo hayo, mapigano hayaonyeshi dalili za kupungua wakati wanapopambana kudhibiti mji wa pili kwa ukubwa nchini humo.

Jeshi la anga la Sudan limeshindwa kuwaondoa wapiganaji wa Rapid Support Forces RSF mjini Khartoum kwani bado wanadhibiti mitaa ya mji huo mkuu huku jeshi likiwa na udhibiti wa mashariki mwa nchi.

Katika kipindi cha miezi mitatu sasa RSF imelidhibiti eneo la mpakani la Om Dafouq na wanaripotiwa pia kuchukua udhibiti wa njia za ziada za usambazaji wa bidhaa kuelekea Kahrtoum.

Marekani na Saudi Arabia zinasema mazungumzo yaliyoanza wiki iliyopita yanalenga kuleta makubaliano ya kusitisha mapigano kwa ajili ya kusambazwa kwa misaada ya kiutu.