1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya watoto walinyanyaswa na Kanisa Katoliki Ureno

14 Februari 2023

Ripoti ya kamati ya wataalamu wanaochunguza unyanyasaji katika Kanisa Katoliki nchini Ureno, imefichua kuwa watoto karibu 5,000 walidhulumiwa kingono katika kipindi cha miaka 70 iliyopita.

https://p.dw.com/p/4NRsq
Sudan | Papst Franziskus in Juba
Picha: Vatican Media/abaca/picture alliance

 Mtaalamu wa magonjwa ya akili yaliepewa jukumu la kuchunguza unyanyasaji huo amesema wengi wa waliotedan dhulma hizo walikuwa makasisi wa kanisa.

Unyanyasaji huo ulifanyika katika maeneo kama vile shule za Kikatoliki na nyumba za makasisi, ambapo kwa mujibu wa ripoti hiyo, waathirika wengi zaidi walikuwa wavulana wasiozidi umri wa miaka 11, mdogo zaidi akiwa na umri wa miaka miwili.

Ripoti hiyo inahimiza hatua za mahakama ya Ureno na msaada wa kisaikolojia kwa waathirika.

Soma pia:Makasisi wa Katoliki Ureno waliwadhulumu kingono watoto 4, 815: Uchunguzi

Kanisa Katoliki nchini Ureno limesema litachukua hatua stahiki kufuatia ripoti hiyo.

Ripoti za vyombo vya habari zinaonyesha kuwa Papa Francis atakutanana baadhi ya wahanga wa unyanyasaji wa kingono wakati wa ziara yake mjini Lisbon mwezi Agosti.

Uchunguzi kama huo umefanyika katika nchi nyingine, kama Australia, Ufaransa, Ujerumani, Ireland na Uholanzi.