1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maelfu ya wasafiri wakwama uwanja wa ndege wa Frankfurt

24 Desemba 2018

Safari za ndege zipatazo 88 zilicheleweshwa katika shirika la ndege la Lufthansa kutokana na eneo la ukaguzi wa usalama kuzidiwa wasafiri, muda wa kusubiri katika eneo hilo la ukaguzi wa usalama ulizidi dakika 90.

https://p.dw.com/p/3Aakz
Deutschland Frankfurt am Main Streik Lufthansa
Picha: DW/J. Michels

Maelfu ya abiria hatimaye waliweza kuondoka siku ya Jumatatu baada ya msongamano mkubwa wa wasafiri mwishoni mwa wiki kwenye eneo la ukaguzi wa usalama katika uwanja huo wa ndege wa Frankfurt hali iliyosababisha safari za watu 3,000 kukosa kusafiri kuelekea kwenye likizo zao. Shirika la ndege ya Ujerumani Lufthansa limelaumiwa mno kwa kutokuwa na wahudumu wa kutosha wakati huu wa kuelekea wa mwishoni mwa mwaka.ambao kwa kawaida huwa na kazi nyingi.

Uhakiki wa usalama kwenye eneo la ukaguzi katika uwanja wa ndege wa Frankfurt, (Terminal 1) ambao linashughulikia safari za kimataifa kuelekea bara Asia na Mashariki ya Kati, ulikumbwa na msongamano mkubwa wa wasafiri ambao walipaswa kusubiri zaidi ya dakika 90 kabla ya kuruhusiwa kuendelea kwenda kwenye maeneo ya kupanda ndege zao.

Kwa mujibu wa shirika la ndege la Lufthansa, hali hii imesababisha ndege 88 kuchelewa kuanza safari zake kwa sababu wasafiri hawakuweza kuyafikia malango yao kwa wakati hatua ambayo ilisababaisha mizigo yao kuondolewa kutoka kwenye ndege.

Ndege za shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa
Ndege za shirika la ndege la Ujerumani LufthansaPicha: picture-alliance/AP Photo/M. Probst

Abiri 50,000 wa ziada

Katika hali ya kawaida, mwishoni mwa wiki, uwanja wa ndege wa Frankfurt huwahudumia kati ya abiria 150,000 na 180,000. LaIkni mwishoni mwa wiki hii, kampuni ya Fraport, inayoendesha shughuli za uwanja huo wa ndege, imekadiriwa kuwa walikuwepo takriban abiria 200,000. Na, imebainika kwamba hapakuwepo na wafanyakazi wa kutosha.

Mkurugenzi mtendaji wa Lufthansa Detlef Kayser amesema amesikitishwa mwishoni mwa wiki kuelekea sikukuu ya Krismasi, kulikuwepo matatizo makubwa katika huduma kwenye uwanja wa ndege wa Frankfurt, amesema mtendaji huyo kwamba anataka masuala yatatuliwe kwa haraka."

Frankfurt imekuwa inakabiliwa na misongamano mikubwa katika maeneo ya ukaguzi wa usalama tangu kipindi cha majira ya joto. Kwa kutafuta suluhisho la tatizo hilo, polisi imefungua kituo cha ziada cha usalama, lakini kitaanza kufanya kazi mwaka ujao wa 2019.

Mwandishi Zainab Aziz

Mhariri: Sekione Kitojo