JamiiArmenia
Maelfu wakimbia Nagorno-Karabakh kwa kuhofia kushambuliwa
29 Septemba 2023Matangazo
Inaripotiwa watu wa jamii ya Armenia walianza kuondoka Nagorno - Karakabakh kuanzia Jumapili na kufikia jana Alhamisi, zaidi ya watu 78,300- ambao ni zaidi ya asilimia 65 ya idadi jumla ya watu 120,000 walikuwa wamehamia Armenia.
Kwa mujibu wa maafisa wa Armenia, watu zaidi wanaendelea kulikimbia jimbo hilo.
Mamlaka za Azerbaijan zimeahidi kuheshimu haki za watu wa jamii ya Armenia, japo makumi kwa maelfu ya wakaazi wa Nagorno - Karakabh wamehama kwa kuhofia kushambuliwa.
Katika miongo mitatu ya migogoro kati ya nchi hizo mbili huku kila mmoja ikimshtumu mwingine kwa mashambulizi, mauaji na aina nyengine ya ukatili, mgogoro huo umewaacha watu katika pande zote mbili wakiishi kwa hofu.