1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Madrid. Hu akaribishwa kwa maandamano ya kupinga haki za binadamu.

14 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEIf

Rais wa China Hu Jintao yuko nchini Hispania katika ziara ya mwisho ya mataifa matatu ya bara la Ulaya.

Kuwasili kwa Hu kumeamsha maandamano nje ya ubalozi wa China mjini Madrid kuhusiana na suala la haki za binadamu nchini mwake.

Siku mbili za mikutano, itaanza leo Jumatatu, ikiwa ni pamoja na mikutano na mfalme Juan Carlos na waziri mkuu Jose Luis Rodriguez Zapatero.

Kabla ya kuwasili kwa Hu nchini Hispania , kiongozi huyo wa China alikuwa kwa muda wa siku tatu nchini Ujerumani , ambako alifanya mazungumzo na maafisa wa Ujerumani na kutia saini makubaliano kadha ya kibiashara.